Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dk Mashinji: Chadema tunawaandaa vijana kuwa viongozi

59751 Pic+chadema

Sun, 26 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Katibu Mkuu Chadema, Dk Vincent Mashinji amesema chama hicho kimewaandaa vyema vijana kushika nafasi za uongozi mwaka 2020.

Dk Mashinji ametoa kauli hiyo baada ya kuulizwa kuhusu kauli iliyotolewa hivi karibuni na Katibu Mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally kuwa matatizo ya viongozi vijana wa sasa yanatokana na chama tawala kutowapika.

Awali, Dk Mashinji alijibu hoja hiyo kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter na alipotakiwa kutoa ufafanuzi alieleza kuwa chama hicho kina programu maalumu ya mafunzo ya uongozi kwa vijana wake na ndiyo sababu wanaonekana kuwa imara na wenye misimamo madhubuti.

Alisema tangu mwaka 2000, Chadema imekuwa ikiwapika vijana wake kupitia programu hiyo inayofahamika kama Leadership Award huku akieleza kuwa imekuwa na matokeo chanya kwa waliopitia.

“Ukiwaangalia wabunge wa Chadema namna wanavyosimamia hoja, wanavyojielezea na jinsi wanavyojiamini, unaweza kuniambia ni chama gani kina watu wa namna hiyo? mfano ukimuangalia Mdee (Halima- mbunge wa Kawe) au Silinde (David- mbunge wa Momba). Hawa wote wamepitia mafunzo haya. Wamefunzwa kwa muda mrefu, lakini sio mtu anakuwa maarufu, amekuwa mpiga kelele kwenye chama cha siasa anakwenda anapewa cheo,” alisema Mashinji.

Chanzo: mwananchi.co.tz