Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dk Biteko awataka wadau wa demokrasia kumiminika bungeni

Biteko Nms.jpeg Dk Biteko awataka wadau wa demokrasia kumiminika bungeni

Fri, 5 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Dar es Salaam. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko amewataka wadau wa demokrasia ya vyama vingi kujitokeza kwa wingi kujitokeza wingi katika mchakato wa utoaji maoni mbele ya kamati za Bunge kuanzia Januari 6, 2024.

Ametoa wito huo leo Alhamisi Januari 4, 2024 wakati akifunga mkutano mkuu maalumu wa Baraza la Vyama vya Siasa ulioshirikisha wadau wa demokrasia kujadili miswada ya sheria za uchaguzi na miswada wa sheria za vyama vya siasa iliyowasilishwa Novemba 10 mwaka 2023.

Mkutano huo maalumu wa siku mbili ulifunguliwa jana Jumatano na Makamu wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Othuman Masoud ukiwa na kauli mbiu,”'toa maoni yako kuimarisha demokrasia” ukishirikisha pia asasi za kiraia, viongozi wa dini na kimila.

"Nichukue nafasi hii kuwaambia muitikie wito wa Spika wa Bunge (Dk Tulia Ackson) aliyewaalika kwenda bungeni kutoa maoni yenu kuanzia Januari 6 hadi 10 bungeni jijini Dodoma, msiache kwenda, haya mlioyazungumza mmejifua vizuri na mmepata mwelekeo.

"Sisi kama Serikali tutayazingatia maoni yenu, lakini muhimu zaidi kwa ajili ya kuzingatia utawala bora utakaoimarisha mhimili wa dola, basi tupate nafasi ya kwenda bungeni kutoa maoni yetu, nawashukuru wote waliotoa maoni yao," amesema Dk Biteko.

Dk Biteko amesema katika mkutano huo washiriki walitoa michango bora, kwa uungwana na kuvumiliana hata yule mjumbe aliyekwenda nje ya mada alipata nafasi ya kusikilizwa.

Amesema majadiliano hayo ni mwendelezo wa kujenga maridhiano yaliyoasisiwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

“Inawezekana una maoni umeyatoa, inawezekana yasichukuliwe yote si dhambi lakini Bunge na kamati lina watu makini watatusikiliza na pale Serikali itakapolazimika kupeleka mabadiliko kwenye muswada itayapeleka ili kuboresha kuwa na sheria nzuri,” amesema Dk Biteko.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge, Sera na Uratibu, Jenista Mhagama amesema Serikali itaongeza juhudi za kuelimisha wananchi kuhusu 4R kwa ajili ya kumuenzi Rais Samia Suluhu Hassan.

4R hizo ni Maridhiano (Reconciliation), mageuzi (Reforms), kujenga upya (Rebuilding) na ustahimilivu (Resilience].

Pia, amesema Serikali itaendelea kuyafanyia kazi maoni ya kikosi kazi cha Baraza la Vyama vya Siasa Tanzania.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live