Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dk Biteko ataka UVCCM kujikita miradi ya maendeleo

Bec477a558d992916541148d4e55d3b9.jpeg Dk Biteko ataka UVCCM kujikita miradi ya maendeleo

Sun, 2 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Madini na Mbunge wa Jimbo la Bukombe, Dk Dotto Biteko ametoa wito kwa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) kuachana na migogoro ndani ya chama na kujikita katika miradi ya maendeleo.

Dk Biteko ameeleza hayo wilayani humo juzi kwenye hafla ya uwekezaji wa jiwe la msingi katika jengo la nyumba ya Katibu wa UVCCM Wilaya ya Bukombe.

Alisema ili vijana na chama waweze kupiga hatua ni lazima wawe mfano bora kwa kuonesha ushirikiano, uwajibikaji na kuweka kando migongano isiyo ya lazima.

“Sisi kiu yetu ni kuona kwamba viongozi wakija waje kuzindua miradi kwenye wilaya yetu ya Bukombe, akija kiongozi wa chama aje kuzindua mradi, siyo aje kusuluhisha mgogoro.

“Moja ya jambo linalotuchelewesha ni kujikita katika migogoro na kujadili majina ya watu badala ya masuala yanayoweza kuwaletea maendeleo watu.

“CCM ni lazima ijibadilishe itoke kwenye mfumo wa kuwa na ajenda ya watu, tuwe na ajenda ya mambo ya kufanya, tuna kundi kubwa la vijana ambao wanahitaji kupata shughuli za kufanya”.

Alisema akinamama na vijana wa CCM wana nafasi ya kutumia fursa ya mikopo ya halmashauri kuweza kuanzisha miradi na biashara yenye tija kwa maendeleo endelevu.

Aidha aliwakumbusha UVCCM na wanachama wote wa CCM wilayani Bukombe kuendelea kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan kuliletea taifa mapinduzi ya miradi.

UVCCM Mkoa wa Geita, Richard Daud alisisitiza “sisi tumejielekeza zaidi kufanya kazi zenye tija kuleta matokeo, ili kukibeba chama chetu na kukiimarisha”.

Mwenyekiti wa Awali akisoma taarifa ya ujenzi wa nyumba ya Katibu UVCCM, Kaimu Katibu wa UVCCM Bukombe, Edmund Ernest alisema hadi sasa wametumua Sh milioni 13 na wanahitaji Sh milioni 15 kuweza kukamilisha ujenzi huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live