Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dk Bashiru azungumzia ushindi wa CCM mwaka 2020

86035 Pic+bashiru Dk Bashiru azungumzia ushindi wa CCM mwaka 2020

Thu, 28 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Unguja. Katibu mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally amesema chama hicho kitashinda kwa kishindo uchaguzi mkuu wa 2020 kama ilivyotokea katika uchaguzi wa Serikali za mitaa uliofanyika Jumapili ya Novemba 24, 2019.

Katika uchaguzi huo CCM imezoa ushindi mitaa yote 4,263 nchini  huku wagombea wake katika mikoa ya Tanga, Katavi, Ruvuma na Njombe wakipita bila kupingwa. Wagombea wa CCM waliopita bila kupingwa nchi nzima ni 316,474.

Dk Bashiru ametoa kauli hiyo leo Jumanne Novemba 26, 2019 kisiwani Zanzibar wakati akizungumza na wazee wa chama hicho katika ofisi kuu ya chama hicho tawala nchini Tanzania.

Amesema matokeo ya uchaguzi huo uliosusiwa na vyama vya upinzani vya Chadema, NCCR-Mageuzi, UPDP, ACT-Wazalendo na CUF,  umebeba tafsiri ya uchaguzi mkuu wa 2020 kwa maelezo kuwa kitashinda kwa kishindo.

Amesema sababu ni kuwa CCM inakubalika kwa wananchi wa rika zote, na kuwataka wanachama wa chama hicho Zanzibar kutobweteka.

Chanzo: mwananchi.co.tz