Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dk Bashiru azungumzia ugumu Kalanga kung’oka Chadema

11387 Pic+bashiru TanzaniaWeb

Sat, 11 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Arusha. Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk Bashiru Ally amesema uamuzi wa aliyekuwa mbunge wa Monduli kwa tiketi ya Chadema, Julius Kalanga kujiuzulu na kuhamia CCM, haukuwa rahisi.

Akizungumza leo Jumamosi Agosti 11, 2018 katika mkutano wa halmashauri ya chama hicho Wilaya ya Monduli, Dk Bashiru amesema ni wazi kuwa uamuzi wa Kalanga ambaye awali alikuwa CCM kurejea tena katika chama hicho tawala haukuwa jambo dogo.

“Unapohama kutoka Chadema kwenda CCM tena kwa nafasi ya mbunge wa Monduli, si jambo dogo haikuwa kazi rahisi. Misingi  ya upinzani imeumia, lakini pia hatua hii imezidi kuiimarisha CCM na Taifa,” amesema.

“Wapo baadhi waliosema eti Kalanga ni muoga amehama usiku, ndugu zangu hizo ni mbinu za kivita za jemedari wetu wakati wengine wamelala wewe unapigana, niwatoe hofu msiogope katika hili.”

Amesema, “Kalanga tunakuunga mkono na tutakuwa pamoja na wewe katika hatua inayofuata kuhakikisha jimbo linarudi CCM.”

Dk Bashiru alihimiza umoja na mshikamano ndani ya CCM ili kuhakikisha chama hicho kinaendelea kushika dola.

Pia atafunga mkutano wa kampeni Kata ya Migungani wilayani Monduli koani Arusha.

Dk Bashiru aliwazima baadhi ya wana-CCM waliokuwa wakipanga kuandamana kupinga Kalanga kuwa mgombea pekee aliyerejesha fomu kuwania kuteuliwa kugombea ubunge Monduli, wakidai kuwa kuna njama zimepangwa.

Chanzo: mwananchi.co.tz