Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dk Bashiru awaita wapinzani, njoo CCM!

13034 Pic+bashiru TanzaniaWeb

Tue, 21 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Zanzibar. Katibu Mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally amesema Tanzania inahitaji vyama vya siasa imara vitakavyolinda na kuhubiri misingi ya utaifa, umoja na mshikamano bila ya kujali tofauti za kisiasa.

Alisema hayo kisiwani Pemba alipokwenda kujitambulisha na kuzungumza na wanachama wa CCM, wilayani Chakechake mkoani Kaskazini Pemba.

Dk Bashiru alisema huu ni wakati wa wapinzani kujitawala kifikra kwa kujiunga na CCM na kwamba, CUF imepoteza mvuto kwa jamii.

Katibu mkuu huyo aliwataka wanaCCM kuwapokea na kuwathamini wanaojiunga na chama hicho kwa kile alichoeleza kuwa wamefanya uamuzi sahihi. Katika mkutano huo aliwapokea wanachama wapya 62 toka CUF.

Naye naibu katibu mkuu wa CCM Zanzibar, Dk Abdulla Juma Saadalla (Mabodi) alisema kazi kubwa ya CCM ni kuwaletea wananchi maendeleo.

Dk Mabodi alitaja miongoni mwa miradi iliyotekelezwa Pemba ikiwamo ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf) na kuongeza bei ya karafuu, kuwa ni utekelezaji sera za CCM.

Awali, mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Pemba, Yussuf Ali Juma alisema wanaendelea na mikakati ya kuhakikisha CCM inashinda ngazi zote katika uchaguzi mkuu ujao.

Chanzo: mwananchi.co.tz