Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dk Bashiru apita katikati makundi CCM

68239 Bashiru+pic

Thu, 25 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Huenda katibu mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally sasa ametulia akisikiliza jinsi hotuba yake inavyotafsiriwa tofauti na makundi yanayoweza kuibuka ndani ya chama hicho baada ya waraka uliotolewa na watangulizi wake wawili.

Na ujumbe wake mkuu wakati akifungua mradi wa maduka ya chama hicho mjini Dodoma juzi ulikuwa ni kuwaonya wanachama wa chama hicho kikongwe kujiepusha na malumbano yanayoendelea aliyoyaita “ya kipuuzi”.

“Ukitaka kujua huu mchezo wa kitoto, wapinzani wameanza kuuchangamkia. Maana wao wanacheza kandimundimu sisi tunacheza viwango vya kimataifa,” alisema.

“ Ukiona wapinzani wamechangamkia porojo na upuuzi ndani ya CCM, ujue hao walioanzisha upuuzi huo hawakitakii mema chama chetu, hawajui taratibu na itikadi ya chama chetu. Mchezo wa kitoto waachie vyama vya upinzani.”

Kauli hiyo inaonekana kama inawalenga walioandika barua hiyo kuwa ndiyo waanzilishi, lakini hotuba yake yote haikutaja neno “barua” wala “makatibu wa zamani” wala “wazee”, ingawa inaonekana kutafsiriwa tofauti na wanachama wanaoonekana kutajwa katika mzozo unaonekana kutamalaki ndani ya chama hicho.

Makatibu hao wa zamani, Abdulrahman Kinana na Yusuf Makamba walilalamikia kuwa uongozi wa chama hauwalindi dhidi ya vitendo vya kudhalilishwa na kuchafuliwa na mtu anayejiita mkereketwa wa Rais John Magufuli.

Pia Soma

Barua hiyo ya Julai 14 inadai kuwa kila mtu sasa anajua kuwa mtetezi huyo anatumwa na watu wenye mamlaka.

Kwa habari zaidi soma gazeti la Mwananchi la leo Alhamisi Julai 25, 2019

Chanzo: mwananchi.co.tz