Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dk Bashiru: CCM tunajipanga kutumia gharama ndogo uchaguzi 2020

86383 Bashirupic Dk Bashiru: CCM tunajipanga kutumia gharama ndogo uchaguzi 2020

Fri, 29 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Unguja. Katibu Mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally amesema chama hicho tawala nchini Tanzania kinajipanga kutumia gharama ndogo katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

Ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Novemba 29, 2019 wakati akizungumza na wajumbe wa kamati za siasa Mkoa wa Kusini Unguja.

Amesema suala hilo litafanikiwa ikiwa watapatikana wagombea wanaokubalika, si kupitisha wagombea kwa sababu ya fedha zao.

Amewataka baadhi ya wajumbe wa kamati za siasa kujiepusha, kutokaa karibu na wenye nia ya kugombea au wenye nyadhifa mbalimbali hivi sasa.

Chanzo: mwananchi.co.tz