Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dk Bashiru Ally amshukia waziri anayemiliki shamba la ekari 1,000

14699 Bashiru+pic TanzaniaWeb

Thu, 30 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Katibu Mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally amesema amemuita mmoja wa mawaziri wa Serikali ya Awamu ya Tano aeleze alipopata ekari 1,000 za mashamba.

Bila kumtaja jina waziri huyo, Dk Bashiru amesema  atamtaka achague jambo moja kati ya kuwa mporaji ama kiongozi wa chama hicho.

Ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Agosti 30, 2018 wakati akifungua mkutano wa Baraza la Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT) Taifa jijini Dodoma.

Amesema mambo yanayozungumzwa katika vyombo vya habari unaweza kudhani ndio hali halisi katika Jamii.

"Viongozi msifanye kazi katika vyombo vya habari nendeni katika maeneo mbalimbali mkatatue kero za wananchi. Nilikwenda eneo moja wananchi wanajiuliza waziri huyo amepataje ardhi hiyo," amesema Dk Bashiru.

Amesema atamuita waziri huyo aeleze amepataje eneo hilo kwa sababu CCM haiwezi kuwa na wanachama ambao ni waporaji wa ardhi.

“Achague kimoja kama ni mporaji ama kuwa kiongozi wa CCM," amesisitiza.

Chanzo: mwananchi.co.tz