Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diwani wa Chadema kata ya Mjimwema ajiuzulu, ahamia CCM

11411 Pic+mji+mwema TanzaniaWeb

Sat, 11 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

 Diwani wa Kata ya Mjimwema Chadema, Selestine Maufi ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo na kujiunga na CCM.

Akizungumza na Mwananchi leo Agosti 11 Katibu wa Chadema Wilaya ya Kigamboni Magese Saimoni amethibitisha kuhama kwa diwani huyo huku akibainisha kuwa huenda wakaendelea kuondoka wengine zaidi.

“Ndiyo ameondoka ni biashara inayoendelea kwenye siasa tuliyonayo sasa, tunamtakia kila kheri huko alipokwenda, sisi tupo busy kuijenga Chadema yetu, wala hajatutingisha maana kaondoka yeye tu labda na mkewe,”amesema Saimon.

Amesema diwani huyo ana miaka minne tangu ajiunge Chadema, awali hakuwa mwanachama wa chama chochote cha kisiasa.  

Hatua ya Diwani huyo ni mwendelezo wa baadhi ya wabunge na madiwani wa vyama vya upinzani kujiuzulu nyadhifa hizo na kujiunga na Chadema.

Hivi karibuni Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala  na Diwani wa Kata ya Vingunguti Omari kumbilamoto alijiuzulu nafasi ya udiwani na umeya lakini pia amejivua uanachama wa Chama cha Wananchi (CUF).

Mwisho

 

Chanzo: mwananchi.co.tz