Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diwani wa Chadema Simanjiro ahamia CCM

Sat, 20 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Simanjiro. Diwani wa Loiborsiret (Chadema), Ezekiel Lesenga amekuwa diwani wa kwanza kumfuata aliyekuwa mbunge wa Simanjiro (Chadema) James Millya aliyejiunga na CCM hivi karibuni.

Lesenga maarufu ‘Mardad’ akizungumza na Mwananchi leo Oktoba 18, 2018 amesema amejiuzulu nafasi hiyo baada ya kuandika barua kwa mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara, Yefred Myenzi.

Amesema amejiuzulu nafasi hiyo ili kumuunga mkono Rais John Magufuli kwani kwa muda wote wa uongozi wake ameshirikiana na Serikali ya awamu ya tano katika kufanikisha maendeleo ya wananchi wa Loiborsiret.

"Najiuzulu udiwani na kuondoka Chadema kwa kujivua uanachama huku nikiachia nafasi zangu zote nilizokuwa nazishikilia na kujiunga na CCM,” amesema Lesenga.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Simanjiro, Yefred Myenzi amethibitisha kupokea barua ya Lesenga kujiuzulu udiwani wa Loiborsiret.

Jimbo la Simanjiro hivi sasa halina mbunge baada ya Millya kujiuzulu nafasi hiyo Oktoba 7, 2018 na kujiunga na CCM.

Awali, Jimbo hilo lenye kata 18, lilikuwa na madiwani 12 kwa tiketi ya CCM na madiwani sita kwa tiketi ya Chadema.

Chanzo: mwananchi.co.tz