Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diwani wa CHADEMA aibuka kinara CCM

Kura CCM.jpeg Diwani wa CHADEMA aibuka kinara CCM

Sun, 25 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wajumbe wa mkutano mkuu wa wilaya ya Bukombe, Mkoa wa Geita wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) wamelazimika kurudia kupiga kura kumpata mwenyekiti wa umoja huo.

Hatua hiyo imetokana na mgombea aliyekuwa akitetea nafasi hiyo, Agnes Sai kutoridhika na kuamini kuwa amepata kura 79 huku mpizani wake wa karibu, Julieth Dibaze akipata kura 126 kati ya wagombea wanne.

Uchaguzo huo imefanyika Jumamosi ya Septemba 24, 2022 na kusimamiwa na Mkuu wa Wilaya ya Bukombe, Said Nkumba.

Nkumba amesema awali kura zilizopigwa 256 na kura 2 ziliihalibika kura halali 254 na kufanya matokeo ya awamu ya kwanza kwa wagombea Asha Ramadhani amepata kura11, Abiba Marushwa amepata kura 38.

Agnes Sai amepata kura 79, huku Julieth Dibaze akipata kura 126 hali ambayo ilimfanya msimamzi kurudia upigaji wa kura baada ya kuridhia wagombea wawili waachiwe mnyukano.

"Hu ni murudio wa mwisho kama kupiga kura wagombea ridhikeni na matokeo ya wajumbe," amesema Nkumba.

Bada ya wajumbe kupiga kura kwa mara ya pili, amemtangaza Julieth Dibaze kuwa mwenyekiti mpya wa UWT wilaya ya Bukombe kwa kupata kura 157 huku Agnes aliyekuwa akitetea akiambulia kura 97 ikiwa kura halali zilikuwa 254.

Julieth amechukua nafasi hiyo na amewahi kuwa diwani viti malumu 2010 hadi 2015 kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na uchaguzi wa 2020 aligombea Udiwani viti malumu kupita CCM kura hazikutosha.

Dibaze akiwashukuru wanawake kwa kumuamini amesema ameamini wanawake wanaweza.

"Nawaahidi kufanya kazi kwa ushirikiano kwa kuimarisha jumuia kwa masilahi ya chama," amesema Dibaze.

Agnes ambaye alishindwa kutetea nafasi yake alisema amepokea matokeo bila kinyongo.

"Asiyekubari kushindwa simshindani nawahakikishia wajumbe naenda kujipanga awamu nyingine na mjue sijachukia mtu," amesema Sai.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live