Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diwani mwingine Chadema ahamia CCM

52842 Pic+diwani

Wed, 17 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Diwani wa Kata ya Chang'ombe  Halmashauri ya Temeke kupitia Chadema, Benjamini Ndalichako amejiuzulu nyadhifa zake zote katika chama hicho na kurejea CCM.

Akitangaza uamuzi wake huo leo, Benjamini amesema  unatokana na maendeleo yanayofanywa na Serikali ya CCM.

Ndarichako amesema amejiuzulu nafasi zote alizokuwa nazi Chadema, kwanza uanachama, pili katibu wa madiwani, mjumbe wa kamati tendaji na mjumbe wa baraza la uongozi la mkoa.

Kwa upande wake,  Meya wa Temeke, Abdallah Chaurembo amesema amefurahia uamuzi wa diwani huyo kurejea CCM.

“Sisi Temeke hatuna malumbano, hatumkatai wala kumfukuza mtu ila tunamrekebisha ili zile kero zinazowakabili ziende kutatulika,” amesema Chaurembo.

Ametoa wito kwa halmashauri nyingine zifike Temeke kujifunza kuendesha miradi kwa gharama nafuu. 

Naye Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva amesema maendeleo ya Temeke ni kwa sababu ya mshikamano wa watumishi na madiwani wa  halmashauri hiyo.



Chanzo: mwananchi.co.tz