Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diwani, mgombea ubunge Chadema atimkia CCM

83851 Pic+diwani Diwani, mgombea ubunge Chadema atimkia CCM

Thu, 14 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanza. Aliyekuwa mgombea ubunge katika uchaguzi mdogo wa Buyungu Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Elia Kanjero amejiengua na kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Kanjero ambaye pia ni Diwani wa Gwarama Wilaya ya Kakonko amejiunga CCM leo Jumatatu Novemba 11, 2019 na kupokelewa na viongozi wa chama hicho tawala wilayani Kakonko wakiongozwa na Mwenyekiti wa wilaya, Saamoja Ndilaliha.

Licha ya msimamo imara usioyumba, Elia aliyejipatia umaarufu kwa kuvaa sare za Chadema katikati ya viongozi na wanachama wa CCM wakati wa ziara ya Rais John Magufuli wilayani Kakonko mwaka 2017 pia alitoa ushindani mkali kwa mbunge wa sasa wa Buyungu (CCM), Christopher Chiza wakati wa uchaguzi mdogo jimbo la Buyungu uliofanyika Agosti 12, 2018.

Akizungumza na Mwananchi kwa simu, Katibu wa CCM mkoa wa Kigoma, Kajoro Vyohoroka amepongeza hatua ya mwanasiasa huyo machachari kuhamia chama tawala na kusema bado kuna orodha ndefu ya viongozi na wanachama wa vyama vya upinzani wanaoomba kuhamia chama hicho.

“Watanzania wakiwemo waliokuwa viongozi na wanachama wa vyama vya upinzani wameridhishwa na utendaji wa Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli,” amesema Vyohoroka

Kwa upande wake, Katibu wa Chadema mkoa wa Kigoma, Shaaban Madede amesema ni haki ya kikatiba na kisheria kwa mtu kujiunga na chama chochote cha siasa anachopenda na kumtakia kila la heri aliyekuwa diwani wao aliyehamia CCM.

Chanzo: mwananchi.co.tz