Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diwani Chadema avuliwa uanachama

58908 Diwanipic

Wed, 22 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Arusha. Kamati ya utendaji ya Chadema Kanda ya Kaskazini imemvua uanachama diwani wa Viti Maalum wa chama hicho, Digna Nassari kwa makosa ya kinidhamu.

Kamati hiyo pia imependekeza Meya mmoja wa jiji anayetokana na chama hicho kuvuliwa uanachama kutokana na makosa ya kinidhamu na usaliti.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumanne Mei 21, 2019, katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini,  Aman Golugwa amesema uamuzi huo umetolewa katika kikao cha kamati hiyo kilichofanyika Mei 18, 2019.

Amesema tayari uamuzi huo umepelekwa ngazi za juu za chama hicho sambamba na hatua za kinidhamu kwa wabunge saba.

Amebainisha kuwa kikao hicho kiliongozwa na Kaimu mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Joseph Selasini ambaye ni mbunge wa Rombo.

Chanzo: mwananchi.co.tz