Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diwani Chadema ajiuzulu, amtaja Dk Tulia

11906 DIWANI+PIC TanzaniaWeb

Sun, 22 Jul 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mbeya. Diwani wa Chadema kata ya Nsalaga jijini Mbeya, mchungaji  David Ngogo amejivua uanachama wa chama hicho kikuu cha upinzani nchini.

 

Amesema amechukua uamuzi huo baada ya kutofautiana na viongozi wa Chadema kuhusu suala la maendeleo, ikiwa ni pamoja na uamuzi wake wa kumuomba Naibu Spika, Dk Tulia Ackson kusaidia maendeleo katika sekta ya elimu katika kata yake.

 

Ngogo ametangaza uamuzi huo leo Jumamosi Julai 21, 2018 na kuieleza MCL Digital kuwa ni vyema akakaa pembeni kuliko kulumbana na viongozi wa Chadema.

 

 

Wakati Ngogo akichukua uamuzi huo, leo uongozi wa chama hicho mkoani Mbeya umependekeza madiwani watatu wa jijini humo kufukuzwa uanachama kwa utovu wa nidhamu na kukiuka taratibu za chama, wakidaiwa kushiriki katika sherehe waliyoalikwa na Dk Tulia mjini Dodoma.

 

Madiwani hao na kata zao kwenye mabano ni  Geofrey Kajigili (Sisimba), Hamphrey Ngalawa (Iwambi) na Newton Mwatujobe (Manga).

 

"Yule (Dk Tulia) ni kiongozi na amekuwa akijitoa kusaidia jamii na sio Mbeya tu hata mikoa mingine. Hivyo na mimi nikamuomba afanye hivyo katika shule iliyopo katika kata yangu. Kweli alifanya hivyo na Alhamisi wiki hii alikuja pale akatoa msaada wa bati 100 na mufuko ya saruji,” amesema.

 

“Lakini katika hafla ya kupokea msaada ule niliwaona viongozi wengine lakini sikuwaona viongozi wanaotokana na Chadema.”

 

Amesema baada ya hafla hiyo ilianza kupokea simu kutoka kwa viongozi wa Chadema wakimlaumu kwa kitendo chake cha kumualika Dk Tulia kwenda katika kata yake.

 

“Ukiona unapingana na kiongozi basi busara zikuongoze kwa kujiweka kando ili kila mmoja abaki na msimamo wake, ndio nilichokifanya,” amesema.

 

“Unapingana na viongozi wako halafu mwaka 2020 utasimama jukwaani kuwaambia wananchi kwamba hukuwaletea maendeleo kwa sababu viongozi wako  hawapendi kuona wageni wanaleta maendeleo? Au utawaambia sikuwaletea maendeleo kwa sababu sikuwa na uhusiano mzuri na viongozi wangu? Watanielewa kweli.”

Chanzo: mwananchi.co.tz