Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diwani CCM apigwa ‘pini’ kushiriki vikao

9473 PIC+DIWANI TanzaniaWeb

Thu, 2 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mbozi. Diwani wa Ipunga Halmashauri ya Mbozi mkoani Songwe (CCM), Barton Sinienga ameamriwa kutoshiriki vikao vitatu vya baraza la madiwani kwa tuhuma za kusema uongo katika kikao.

Akitoa uamuzi huo kwenye kikao cha baraza hilo juzi, mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Erick Ambakisye alisema kutokana na kukiuka kanuni za baraza hilo kwa kusema uongo diwani huyo amefungiwa kutoshiriki vikao vitatu kuanzia Julai 30.

Pia, diwani huyo atapoteza stahiki zake zote za udiwani na kuwa kwa tafsiri hiyo atatumikia adhabu hiyo hadi Julai mwakani.

Alisema diwani huyo alitenda kosa hilo baada ya kudai katika halmashauri hiyo kuna upotevu wa Sh1.2 bilioni zilizotokana na ushuru wa mauzo ya kahawa msimu 2016/17 na Sh17 milioni zilizotolewa kama mgawo wa asilimia 20 ya mapato ya halmashauri, ambazo zilitakiwa kupelekwa mamlaka ya mji mdogo wa Vwawa.

Diwani huyo ni wapili kuchukuliwa hatua kama hiyo tangu baraza hilo kuingia madarakani 2015, mwaka jana diwani wa Mlowo (Chadema), Sebastian Kilindu alifungiwa kushiriki vikao vitatu na adhabu yake ilimalizika juzi kwa kosa kama hilo.

Ambakisye alisema diwani huyo aliwasilisha vielelezo ambavyo vinaonyesha alikokotoa hesabu za ushuru wa kahawa kutokana na mauzo ya mnadani kwa kutumia viwango vya fedha za kigeni, badala ya bei ya shambani ambayo ndiyo inatumika kisheria ambayo ni asilimia tatu ya bei.

Akitoa utetezi wake, Sinienga alisema ana uhakika vielelezo alivyowasilisha ndivyo vinavyotumika kukata ushuru kutoka kwa wakulima na vikundi vingi vimekuwa vikikatwa kwa gharama hiyo.

Chanzo: mwananchi.co.tz