Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diwani CCM aliyefukia kisima cha wananchi ajisalimisha

Shigongo 12 Diwani CCM aliyefukia kisima cha wananchi ajisalimisha

Fri, 5 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Diwani wa Kata ya Irenza Mneke Mauna (CCM) aliyetuhumiwa na wananchi wa kitongiji cha Nyangalamila B Kijiji cha Nyangalamila Kata ya Irenza Halmashauri ya Buchosa Wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza kufukia  kisima walichopewa fedha na mbunge wa Jimbo hilo, Eric Shigongo hatimaye amejisalimisha ili wafanye kazi pamoja.

Tukio hilo limejitokeza kwenye mkutano wa hadhata wa Mbunge wa Buchosa  Mhe. Eric Shigongo uliofanyika Kijiji cha Ilenza kata Irenza wilayani huko ambapo alimwomba mbunge huyo waendelee kushirikiana kwa pamoja ili kuwaletea wananchi maendeleo

”Tusahau yaliyopita tunapaswa kusonga mbele tuwatumike wananchi wetu waliotuchagua Mimi na wewe tuweke tofauti zetu pembeni tuwasaidie wananchi, amesema  Mneke akiwa  kwenye mkutano wa hadhata .

Machi 27,2023 mwaka Jana  wananchi wa kitongiji cha Nyangalamila B Kijiji cha Nyangalamila Kata ya Irenza waliandamana baada ya diwani wa Kata hiyo kufukia kisima walichopewa fedha na mbunge  hali iliyoleta taharuki kubwa na kutokuelewana na mbunge.

Baada ya tukio la kufukiwa kwa kisima hicho mbunge wa Buchosa Eric Shingongo alifanya jitihada kama mwakilishi wa  wananchi wa Jimbo kuhakisha wananchi wa kitongiji cha Nyangalamila B kata ya Ilenza kupata kisima ambayo kitawasaidia kupata maji safi na salama .

Kupitia Wiraza ya maji , Mamulaka ya maji safi na usafi wa mazingira vijiji Wilayani Sangerema (Ruwasa) walichimba kisima kirefu cha maji kwenye kitongiji hicho chenye thamani ya Sh42milioni ambacho kimekisha malizika  na wananchi wanapata huduma ya maji.

Kwa upande wake mbunge wa Buchosa Eric Shigongo amewaambia wananchi

kuwa tofauti zao zimeisha hivyo amewaomba wananchi kuwaunga mkono ili kutekeleza Ilani ya CCM kwa kuwaletea maendeleo wananchi wa Kata ya irenza na wakazi wa Buchosa Kwa ujumla.

“Nichukue nafsi hii kumshukuru diwani wenu kwa kazi nzuri aliyoifanya niwaombe wananchi waka kata ya irenza mtuunge mkono tuwaletee maendeleo tofauti zetu zimeisha sasa tusimama pamoja kutekeleza Ilani ya chama chetu,amesema Shigongo.

Baadhi ya wananchi wa Kata ya Irenza waliokuwa kwenye mkutano wa hadhara wamepongeza hatua ya diwani wa Kata hiyo Mneke Mauna kumaliza tofauti na mbunge wake ili wananchi wa Irenza tuweze kupata maendeleo.

Kefline Kitambi mmoja wa Kazi wa Kijiji cha Irenza amesema sasa kata ya Irenza itapata maendeleo kwa kasi baada ya diwani kutambua kuwa kufanya  kazi na mbunge mtafuta pesa za maendeleo jimboni nijambo la hekima na busara.

Wananchi wa Kata ya Irenza Halmashauri ya Buchosa Wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza wamepongeza hatua ya diwani wa Kata ya Irenza  Mneke Mauna kujisalimisha na kuendelea kufanya kazi na Mbunge wake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live