Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Kisarawe, Khamisi Dibibi amebidhi vifaa vya ofisi za Jumuiya kwa Makatibu kata na matawi vyenye thamani ya zaidi ya shillingi milioni 9 ikiwa ni mkakati wa kukijenga Chama cha Mapinduzi Wilayani humo.
Vifaa alivyokabidhi Dibidi ni viakisi mwanga kwa Viongozi wote wa kata za Wilaya ya Kisarawe, Kadi za jumuiya ya wazazi 300 kila tawi kwa matawi 119, stap pad (Kidawu) kwa matawi yote 119 na kata 17.
Dibibi pia alikabidhi reja za kusajiria wanachama kwa matawi yote 119, mihuliya matawi yote 119 na kata zote 17, mbele ya mkutano huo wa Jumuiya hiyo ngazi ya wilaya, ambapo Kaimu Katibu wa Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Pwani, Sophia Abdul alikuwa ni Mgeni rasmi.
Dibibi amewataka Makatibu kata na matawi kuanza maandazi ya chaguzi za serikali za mitaa kwa kuhimiza wenye sifa kujitokeza kuchukua fomu za kugombea Uongozi muda utakapofika.