Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Demokrasia yawakimbiza CHADEMA

CHADEMA Vs CCM Wawili watimkia CCM kutoka Chadema

Tue, 3 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wanachama wawili wa Chadema mkoani Singida wamehama chama hicho na kujiunga na CCM, kwa madai kukosekana kwa demokrasia halisi wanayoinadi viongozi wao kila siku.

Wanachama wawili wa chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA,ndugu Philemoni Ghula ambaye alikuwa kampeni meneja wa kata ya Unyahati na Julius Sunna aliyekuwa mgombea Udiwani kata ya Mkingu, wamehamia chama cha Mapinduzi CCM wakidai wameifuita demokrasia ya kweli inayopatikana kwenye chama hicho

Akizungumza mara baada ya uamuzi huo Ghula amesema wamechukua uamuzi huo ili kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan.

"Rais Samia anafanya kazi nzuri sana inayoonekana na kila mmoja wetu hivyo tuna kila sababu ya kumuunga mkono," amesema Ghula.

Kwa upande wake Sunna amesema amechukua uamuzi huo kutokana na kuchoshwa na ubabaishaji wa viongozi wao wasiotaka maendeleo ya wananchi.

"Sisi tumetumikia Chadema kwa miaka mingi tena kwa kujitolea, lakini hawakutambua thamani na mchango wetu," amesema Sunna.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ikungi, Mika Likapakapa amewapongeza wanachama hao wapya na kuwakaribisha wakijenge chama na nchi ili kuchochea maendeleo ya wananchi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live