Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dar es Salaam kufanya uchaguzi mitaa miwili pekee

84943 Uchaguzi+pic

Thu, 21 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Wakati shughuli za kampeni za uchaguzi wa Serikali za mitaa zikiendelea katika mikoa mbalimbali, Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema uchaguzi huo utafanyika katika mitaa miwili kati ya 576.

Makonda alisema hatua hiyo inatokana na mitaa yote iliyobaki wagombea wa CCM, kupita bila kupingwa.

“Watu wameamua wenyewe kuunga mkono, wanaona kama kila kitu kinafanywa kwa ubora na serikali ya Magufuli,” alisema.

Alitoa kauli jana alipozungumza na viongozi wa dini katika mkutano uliolenga la kuwaeleza miradi iliyotekelezwa na Serikali ya awamu ya tano tangu iingie madarakari mwaka 2015.

Wakati huo huo, baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani vitakavyoshiriki uchaguzi huo wameeleza jinsi watakavyoshiriki kampeni.

Vyama hivyo ni ADC, NRA, Demokrasia Makini, TLP, DP na AAFP. Chama cha NLD kipo katika sintofahamu baada ya viongozi wake kuvutana kuhusu kushiriki uchaguzi huo utakaofanyika Novemba 24.

Pia Soma

Advertisement
Wakati vyama hivyo vikipanga mikakati, vyama vingine saba; CUF, Chadema, NCCR-Mageuzi , ACT-Wazalendo, UPDP na Chaumma vimejitoa.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Mwananchi, Abdul Mluya, Katibu Mkuu wa DP alisema, “tumezindua kampeni zetu jana mkoani Kigoma ambako tuna wagombea saba ngazi ya vijiji.”

Alisema watafanya kampeni za jukwaani , nyumba kwa nyumba na mtu kwa mtu ili tuwafikie wananchi wote wa mtaa husika.

Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia Makini, Mohamed Abdula alisema watazindua kampeni Novemba 21 mkoani Morogoro.

Katibu Mkuu wa NRA, Hassan Kisabya alisema watafanya kampeni za jukwaani na nyumba kwa nyumba hasa mkoani Kigoma.

Chanzo: mwananchi.co.tz