Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DKT. BASHIRU ATOA NENO KWA WAGOMBEA CCM

Image 495.png?fit=536%2C397 DKT. BASHIRU ATOA NENO KWA WAGOMBEA CCM

Mon, 7 Sep 2020 Chanzo: zanzibar24.co.tz

Wakati vyama mbalimbali vikiendelea na kampeni za kunadi sera zao kwa wananchi kuelekea Oktoba 28, 2020, Chama cha Mapinduzi (CCM) kimepiga marufuku wagombea wake kutoka majimboni mwao pasi na idhini ya Kamati ya Siasa ya Wilaya ya chama hicho.

Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru Ally ametoa maagizo hayo kupitia ukurasa wa Twitter wa chama hicho, huku akiwataka wagombea kufuata ratiba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na kamati za siasa.

“Tuwatafutie kura wagombea udiwani na mgombea Urais. Tufafanue ilani yetu tuliyotekeleza na kilichobaki na kuhamasisha wanachi kupiga kura,” amesema Dkt. Bashiru Ally.

Chanzo: zanzibar24.co.tz