Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chongolo awasili Burundi, kushiriki sherehe za kuzindua uwanja

IMG 20220624 WA0422 Chongolo awasili Burundi, kushiriki sherehe za kuzindua uwanja

Sat, 25 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo amewasili nchini Burudi kwa ajili ya kudumisha uhusiano na Chama cha CNDD FDD cha nchini humo.

Chongo alivyowasili, alipokelewa na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha CNDD FDD Ndugu Ntakarutimana Joseph alipofika Mugina mkoani Makamba, Burundi.

Katibu Mkuu ameongozana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar) Dkt. Abdullah Juma Saadallah pamoja na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga kwa ziara ya kuimarisha uhusiano wa vyama hivyo viwili pamoja na kuhudhuria sherehe za uzinduzi wa uwanja wa kisasa wa michezo wa Nkurunziza Peace Park Complex zitakazofanyika leo Juni 25, 2022.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live