Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chongolo atoa maelekezo skimu za umwagiliaji Bahi

Chongolo Atoa Maelekezo Skimu Za Umwagiliaji Bahi.jpeg Chongolo atoa maelekezo skimu za umwagiliaji Bahi

Wed, 21 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi( CCM) Daniel Chongolo ameiagiza Wizara ya ya Kilimo,Mkuu wa Mkoa pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Bahi kukaa pamoja kuangalia namna ya kupata ufumbuzi wa changamoto ya kukwama kwa miradi ya Skimu za kilimo cha umwagiliaji.

Chongolo ametoa maelekezo hayo akiwa katika ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025 pamoja na kukagua uhai wa Chama hicho sambamba na kusikiliza kero za wananchi na kuzipatia ufumbuzi.

Akizungumza na wananchi wa Bahi katika mkutano wa kawaida wa Shina namba 18, tawi la Bahi katika Kata ya Bahi, Chongolo amepokea changamoto ya kuharibika kwa Skimu za umwagiliaji na hadi sasa hakuna ukarabati uliofanyika au kutengenezwa.

"Na mimi niagize Wizara ya Kilimo, watalaamu wametueleza kwamba watafanya upembuzi yakinifu sijui uchoraji na upimaji na kila kitu mpaka huku lakini hawajashuka kuja kuzungumza nao kuwaeleza wanataka kufanyaje na lini.

"Sasa niwaagize hapa watu mkutane na mkuu wa wilaya, Mkuu wa mkoa pamoja na timu ya Wilaya ya Bahi wawape hicho wanachotaka kufanya wasikilize maoni yao na wakusanye pamoja na kisha wamkabidhi Waziri wa Kilimo kwa niaba ya wakulima ili baada ya hapo tupate ufumbuzi, " amesema Katibu Mkuu Chongolo.

Awali wakati akizungumza na wananchi hao Chongolo amesema amewasikia wakizungumza kuhusu skimu za umwagiliaji na kwamba wamepata fedha kidogo kama Sh.bilioni tano lakini wamemtajia na skimu nyingine nne za Matangira, Uherera, Mtazamo na Nguvu mali

"Mmezitaja hizi skimu na skimu hizi ni za muda mrefu mnachoomba ili mambo yawanyookee ni fedha zitengwe ili zifanyiwe ukarabati.Lakini watalaam mpo hapa hizo skimu mnazijua hakikisheni mnazitengeneza na ikiwezekana zijengwe upya badala ya kufanya matengenezo.

"Nimemuita mtalaam hapa azungumze na ninyi ili mumsikie wenyewe akisema.Niwaambie kuanzia wiki ijayo yaani Julai 1 mwaka huu maelekezo yetu kwa Serikali Skimu 22 ambazo zimetengewa zaidi ya Sh.bilioni 290 pamoja na skimu nyingine ambazo zimetengewa zaidi ya Sh. bilioni 100 ambazo zinaenda kwenye Skimu...

"Na nyingine ambazo zinaenda kukarabatiwa na nyingine kufanyiwa upembuzi yakinifu na mambo mengine wahakikishe zinatangazwa haraka.Lengo la kuzitangaza haraka ni nini?zikishatangazwa zikaenda kwenye manunuzi maana yake uhakika wa kumpata mkandarasi mapema unakuwepo .

"Na skimu kama hizo ndogo ndogo mnazitaja zikiendelea kukarabatiwa haziwezi kuwa bora kama zikijengwa upya, zikijengwa upya kwa mchoro najua zitakuwa zimeongeza hata ukubwa, " amesema Chongolo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live