Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chongolo ataka viongozi Serikali za Mitaa wachunguzwe Dodoma

Chongolo Amtaka Mchengerwa Kushughulikia Mgogoro Ruaha.jpeg Chongolo ataka viongozi Serikali za Mitaa wachunguzwe Dodoma

Mon, 26 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo amesema ili kutatua changamoto ya migogoro ya ardhi katika Jiji la Dodoma na Mkoa kwa ujumla atakutana na Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) huku pia akitaka uchunguzi ufanyike kwa viongozi wa Serikali za Mitaa na Vijijini kwani wengi wao ndio wanaosababisha migogoro hiyo.

Chongolo ameyasema hayo mbele ya wananchi wa Jiji la Dodoma akiwa katika siku ya mwisho ya kuhitimisha ziara yake katika Mkoa wa Dodoma baada ya kutembelea Wilaya zote na Kisha kuimalizia katika Jiji hilo.

"Changamoto na migororo ya ardhi Dodoma imekuwa kubwa na hakuna mgogoro wa ardhi ambao unakuja hauna sababu, sababu na hatuwezi kuzungumza migogoro ya ardhi bila kuwazungumzia wasababishaji na wanaosababisha ni miongoni mwetu sisi hawatoki mbinguni ,sio malaika.

"Na wala sio mitume,ni wananchi ,wanadamu na baadhi yao unakuta wamepewa dhamana ya kuwa watendaji kwa niaba ya wananchi,kuwa viongozi kwa niaba ya wananchi. Ukiona migogoro ya ardhi popote basi kuna watu wamebadilika badala ya kuwahudumia wananchi wanahudumia matumbo yao tena kwa rushes,"amesema Chongolo.

Amefafanua " Nawengi wao wako kwenye ngazi za chini ndio mabingwa ,ukiangalia kwenye levo ya Mkurugenzi wa Halmashauri ,Manispaa Jiji,ukiangalia levo ya Wizara unakuta pale chini ndio kwenye chanzo cha migogoro.

"Kuna Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa, kuna Mtendaji wa Serikali ya Mtaa , mpaka mgogoro unatoka pale unaenda sehemu nyingine yeye anafanyaje?Kama yuko kwenye sehemu yake,kwanini utokee mgogoro,kwa hiyo kwanza kwa tatizo la Dodoma hatua za Kwanza za kufanya ni kufanya uchunguzi wa kina

"Kuhusu watendaji wa Serikali za mitaa wote kwenye Mkoa na Jiji la Dodoma na hili naiagiza Wizara ya TAMISEMI,nitaenda kukaa nao ,katika mambo makubwa tutakayofanya ,Sasa hivi acheni itoshe kusema nimeyasikia ,nimeyachukua turuhusuni twendeni tukayafanyie kazi,"amesema Chongolo.

Ameongeza mpaka imefikia kuitwa migogoro maana yake kuna jambo kubwa la kujifunza hivyo lazima waangalie hapo chini ,kuna watu wanaotimiza wajibu wao? lasivyo wachukue watalaam wa ardhi au watalaam wa mipango miji au watalaam wa upimaji na ramani au wawekwe wanajeshi wawe watendaji wa mitaa yote

Amesema kukiwa na watu ambao wanataaluma inayoendana na changamoto tutatua tatizo Hilo la tatizo la migogoro ya ardhi ambalo ndilo tatizo kubwa hapa nchini.Ofisi ya Serikali ya Mtaa ndio imebadilika kuwa inawauzaji wa viwanja , ndio madalali.

"Halafu ukitoka hapo unaona wanakuja levo ya Kata na baadhi ya madiwani unakuta wamo ndani.Ukitoka hapo sasa unakuja kwenye migogoro ya juu ngazi ya Wilaya ile migogoro inayohusu shughuli za maendeleo ya nchi, shughuli za migogoro ya Serikali,hiyo ndio migogoro tuna dhamana ya kuitekeleza na kuitatua kwa levo yetu."

Hata hivyo amesema lakini maeneo yenye manung'uniko ni hiyo iliyopo ngazi ya chini inayohusu mtu na mtu na wengi wanaosababisha wako kwenye ngazi hizo za chini "Huku juu tutawaonea ,labda kwasababu wanabeba dhamana ,dhambi na msalaba kwasababu wanaotenda kule chini ni wa kwao

"Nimepewa dhamana ya kusimamia Serikali ,tuacheni tukafanyie kazi.Hapa inatakiwa tufanye operesheni maalum ,hapa ni makao makuu ya nchi ,heshima ya makao makuu haziwezi kuwa migogoro ya ardhi,lazima iwe ya hadhi inayoendana na jina lake."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live