Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chongolo ataka maoni ya wananchi kuhusu bandari yakusanywe

Tanzania Ipo Kwenye Vita Ya Kiuchumi   Chongolo.jpeg Chongolo ataka maoni ya wananchi kuhusu bandari yakusanywe

Thu, 20 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katibu mkuu wa Chama cha Mapindizi (CCM) Daniel Chongolo ametaka Maoni ya Wananchi kuhusiana na Mjadala wa Uwekezaji na Uendelezaji wa Bandari yaanze kukusanywa, ambapo yale ambayo yataonekana kuwa na tija ndio yatakayofanyiwa kazi.

Komredi Daniel Chongolo ametoka Kauli hiyo leo Wilayani Korogwe mkoani Tanga katika mkutano wake wa Hadhara wakati alipokuwa akielezea usahihi wa Makubaliano ya Mkataba wa Uwekezaji wa Bandari hapa nchini.

"Sisi tumesema maoni ya Wananchi yakusanywe, yale yenye tija yaingizwe kwenye Mjadala na Kwenye mkataba utakaoingiwa kwa ajili ya Uendeshaji wa Bandari au Sehemu ya Bandari yetu" amesema Chongolo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live