Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chongolo aongoza harambee KKKT Mafinga, wakusanya Sh220 milioni

Chongolo KKKT.jpeg Chongolo aongoza harambee KKKT Mafinga, wakusanya Sh220 milioni

Sun, 25 Sep 2022 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo amefanya harambee ya ujenzi wa kanisa la KKKT usharika wa Mafinga na kufanikiwa kukusanya Sh220 milioni kwenye harambee hiyo.

Akizungumza katika hafla fupi kwa ajili ya harambee ya kukamilisha ujenzi wa kanisa hilo, Chongolo amesema kuwa kwa niaba ya Serikali na Chama wameweza kuwakilisha mchongo wa Sh40 milioni ili kuunga mkono ujenzi huo.

Katibu mkuu huyo ameushukuru uongozi wa kanisa hilo kwa kuona umuhimu wake na kumualika kwa ajili ya kufanya harambee hiyo ili kuweza kukamilisha ujenzi wa kanisa hilo.

"Nashukuru kwa mwaliko huu nitaendelea kuzungumza na wadau mbalimbali ambao wameonyesha Moyo wa kuunga mkono kwa ajili ya jambo hili hivyo nitakamilisha kwa wale wote waliohaidi nitakusanya fedha hizo na kuziwasilisha." amesema Chongolo

Kwa upande wake mchungaji wa kanisa hilo, Dk Anthony Kipangu amesema kuwa wanamshuru Mungu kwa kuweza kufanikisha siku hiyo ya shughuli ya uchangiaji wa kanisa hilo.

Aidha amesema kuwa aendelee kuwapa hekima kwa nafasi ambayo wameipata kwa ajili ya kuongoza Chama cha Mapinduzi ambacho ndio kinaongoza kwa sasa kwa hekima za Mungu aijalie nchi yetu iendelee vizuri kuwa na amani na upendo.

"Chongolo ni kiongozi ambaye ataweza kumshauri Rais wa Samia Suluhu Hassan mambo yaliyomema mengi sisi kama kanisa tunaahidi kushirikiana na Serikali kufanya mambo ya maendeleo." Amesema Dk Kipangula.

Amesema kubwa kazi sio kuwahubiria wahubiri washiriki na kuwabadili na kuwafundisha katika kujikwamua katika magumuĀ  ambayo wamekuwa wakikutana nayo sanjari na katika mambo ya kiuchumi.

Mbali na hilo pia viongozi hao wa dini wa kanisa hilo wamefanya maombi kwa lengo la kuwaombea viongozi wa nchi na kaifa kwa ujumla ili Mungu aweze kuwaongoza katika utendaji wao wa kazi katika kuwatumia watanzania.

Awali akisoma taarifa ya ujenzi huo katibu wa Ujenzi wa kanisa hilo, Hazron Myinga amesema baada ya harambee hiyo matarajio yao kanisa hilo likamilike mapema ili christmas ya mwaka huu liweze kutumika.

"Lengo la harambee hii kukusanya si chini ya Sh250 milioni ili kukamilisha kazi zifuatazo na kuziwezesha kanisa kuanza kutumika hivyo katika harambee watashiriki wageni mbalimbali ambao tuliwaalika kwa ajili ya kushirikiana na katibu Mkuu kumuunga Mkono kwa ajili ya zoezi hili." amesema Myinga

Chanzo: www.mwananchi.co.tz