Imethibitika kuwa Barua kwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa, Samia Sulu Hassan ya Kujiuzulu nafasi ya Katibu Mkuu CCM iliyosambaa mtandaoni ni ya kweli na iliandikwa na Daniel Chongolo.
Katika Barua hiyo Chongolo ameeleza uamuzi wake wa Kujiuzulu ni kutokana na kuchafuliwa katika Mitandao ya Kijamii siku chache zilizopita ambapo amesema imemkumbusha Kuwajibika kama Kiongozi.
Aidha, kumekuwepo na taarifa za kuwa amepata ajali, imethibitika kuwa gari hilo la ofisi ya Katibu Mkuu wa CCM lilipata ajali kati ya Machi 2023 na sio tukio la hivi karibuni.
CCM bado haijatoa tamko lolote kuhusu barua hiyo huku taarifa za ndani zikieleza kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara, Said Mtanda, na Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Anthony Mtaka, wanatajwa kuwa miongoni mwa orodha ya viongozi na makada wa CCM wanaoweza kumrithi Chongolo kwenye nafasi hiyo.