Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chongolo ampa maagizo Naibu Waziri Mkuu Dk Doto Biteko

Tanzania Ipo Kwenye Vita Ya Kiuchumi   Chongolo.jpeg Chongolo ampa maagizo Naibu Waziri Mkuu Dk Doto Biteko

Tue, 3 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo amewataka mawaziri wanne akiwemo, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko kushughulikia kero zilizoibuliwa na wananchi na viongozi kwenye ziara yake za umeme, maji na huduma za afya mkoani Katavi.

Mawaziri wengine na wizara zao kwenye mabano ni, Jumaa Aweso (Maji), Innocent Bashungwa (Ujenzi) na Mohamed Mchengerwa wa Ofisi ya Rais- Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi).

Kero hizo zimeibuliwa leo Jumanne, Oktoba 3, 2023 katika siku ya kwanza kati ya tano ya ziara ya Chongolo mkoani Katavi, akiwa Wilaya ya Tanganyika kukagua uhai wa chama na utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya mwaka 2020/25.

Dk Biteko anapaswa kwenda kuangalia na kufuatilia kwa kina kujua sababu za mkoa huo kutokuwa kwenye gridi ya Taifa. Chongolo amesema, kwa mamlaka aliyonayo waziri huyo anaweza kulisimamia.

Waziri Bashungwa yeye ahakikishe wakandarasi wawili watakaojenga barabara ya kwenda Bandari ya Karema kilomita 112 muda utakapofika wa kusainiana mikataba ya utekelezaji, shughuli hiyo ikafanyikie Karema na si Dar es Salaam ili wananchi washuhudie wenyewe.

Kwa upande wa Waziri Aweso, ndani ya wiki mbili anapaswa kwenda wilayani Tanganyika kufuatilia mradi wa maji unaosuasua. Mradi huo wa zaidi ya Sh1 bilioni, umefikia asilimia 45 huku mkandarasi anayeutekeleza akiwa hajalipwa fedha.

Waziri wa nne ni Mchengerwa ambaye amepewa jukumu la kutafuta watumishi maeneo mengine nchini na kuwapeleka wilayani Tanganyika kwenye uhaba ikiwemo Hospitali teule ya wilaya hiyo, iliyojengwa Kata ya Ikola.

Pia, Waziri Mchengerwa asimamia upatikanaji wa fedha zitakazokwenda kumalizia hospitali hiyo.

Chongolo amesema yeye akiwa msaidizi wa Mwenyekiti wa chama hicho, Rais Samia Suluhu Hassan anawajibu wa kusimamia na kufuatilia ahadi na utekelezaji wa ilani ya chama.

Amesema mengine atayabeba,"na nikirudi nitakwenda kumwona Rais na kumweleza nilichokiona na kupewa changamoto zenu wananchi."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live