Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chongolo: Waliohudhuria Mkutano Mkuu ni 1928

CHONGOLLOOO 111 Chongolo: Waliohudhuria Mkutano Mkuu ni 1928

Wed, 7 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Daniel Chongolo amesema kuwa idadi ya wajumbe waliyoudhuria mkutano mkuu wa 10 wa CCM ni 1928 sawa na asilimia 99.6 ya wanachama.

Katika mkutano huo wajumbe wa mkutano mkuu watachagua viongozi mbalimbali wa chama wa CCM akiwemo Mwenyekiti wa chama Taifa, ambapo jina lililopendekezwa ni la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Jumla ya wagombea 251 wanagombea nafasi15 upande wa bara na wagombea 123 wanagombea nafasi 15 upande wa Zanzibar.

Lakini pia Mhe. Chongolo ameeleza kuwa Zaidi ya wanachama milioni moja wa chama hicho wamejitokeza kuombanafsi mbalimbali ndani ya chama hicho katika zoezi la uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live