Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chongolo: Viongozi walalamishi wanatuchelewesha

Chongolo Dan Chongolo: Viongozi walalamishi wanatuchelewesha

Tue, 24 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo amewataka Viongozi mbalimbali walioteuliwa Serikalini kufanya maamuzi badala ya kuwa Watu wa kulalamika huku akisisitiza kuwa watachukua hatua kwa wale ambao wataonekana hawaendi sawa na Chama kinavyotaka.

Katibu Mkuu Chongolo ameyasema hayo leo January 24, 2023 Jijini Dodoma wakati wa mapokezi ya Wajumbe wa Sekretarieti mpya ya CCM Taifa ambapo amesema wanashangaa kuona baadhi ya Viongozi wakiwemo Mawaziri, Wakuu wa Mikoa na Viongozi wengine wanalalamika kutopewa ushirikiano na Watumishi wa chini yao, hivyo amewataka wajitathmini wao wenyewe kama wanatosha kwenye nafasi hizo.

" Unamkuta Mkuu wa Mkoa badala ya kufanya kazi analalamika, Mkuu wa Wilaya naye analalamika, tupo kwenye wakati wa kutenda, tuna hitaji viongozi wajue wana dhamna, wamepewa vipande vya kutumikia, sasa usipofanya maamuzi unatuchelewesha kufikia malengo yetu" Amesema Katibu huyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live