Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chongolo, Shaka wamtembelea Profesa Jay

P Jayyyy Chongolo, Shaka wamtembelea Profesa Jay

Thu, 10 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka wamemtembelea aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Mikumi, Joseph Leonard Haule maarufu Profesa Jay aliyelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) akipatiwa matibabu.

Profesa Jay ambaye msanii nguli wa kizazi kipya amelazwa Muhimbili kwa zaidi ya mwezi sasa.

Akizungumza hospitalini hapo leo Alhamisi Februari 10, 2022 baada ya kumuona msanii huyo, Chongolo amesema kuwa hali yake inaendelea kuimarika.

Amesema "Tumemuona ndugu yetu (Prof Jay) hali yake inazidi kuimarika, tumshukuru Mungu lakini niwashukuru madaktari kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kumhudumia lakini kwa Niaba ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Samia Suluhu Hassan niwahakikishie tutaendelea kutoa kila aina ya ushirikiano katika kuhakikisha matibabu yanaendelea vyema huku tukiendelea kumuombea apone haraka" amesema Chongolo.

Viongozi hao wa CCM wamefika hospitalini hapo ikiwa ni siku moja baada ya kuanzishwa kampeni kwenye mitandao ya kuchangia matibabu ya masanii huyo.

Jana, katika mitandao ya kijamii lilisambaa tangazo likiomba kuchangia matibabu ya msanii huyo ambapo pia mkewe wake Profesa Jay, Grace Mgonjo alithibitisha kuwa wameruhusu michango hiyo huku akieleza kuwa kwa wiki moja wanatumia mpaka Sh4 milioni katika matibabu yake hivyo wameona watoe nafasi kwa watu wake kumchangia matibabu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live