Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chongolo: Marufuku kujibebesha mamlaka ya chama

Chongolo Pic Data Daniel Chongolo, Katibu MKu CCM Taifa

Wed, 1 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimepiga marufuku wanachama wake kujibebesha mamlaka na kujimilikisha chama kinyume na katiba ya chama.

Akizungumza wilayani Maswa mkoani Simiyu, Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo amesema chama ni kikubwa kuliko mtu na kila mmoja ana nhaki sawa ndani ya chama na hakuna mkubwa kuliko mwingine.

Chongolo ametoa kauli hiyo katika ziara yake ya kukagua uhai wa chama na kuangalia utekelezaji wa ilani ya chama kwa serikali kwenye miradi ya maendeleo.

"Niwaonye wanachama wa CCM ni marufuku mwanachama kujibebesha mamlaka au kujimilikisha chama,hiki chama sio cha mtu na hakuna aliyemkubwa kuliko chama hata mimi nalipa ada ya uanachama sawa na wanachama wengine,kila mmoja ana haki sawa,"amesema Chongolo.

Aidha, amekemea tabia ya baadhi ya wana CCM kujipitisha pitisha kwa wanachama kutengeneza fitna dhidi ya viongozi wa chama walio kwenye nafasi za uongozi na kusema chama kwa sasa nafasi zimejaa,hivyo wasubiri wakati ukifika watatangaza nafasi ili waombe .

Chongolo amesema viongozi wa chama waliopo madarakani waachwe wafanye kazi zao za kuletea wananchi maendeleo na kusema fitna zinazopitishwa chini chini kwa wanachama dhidi ya viongozi hao zinarudisha nyuma maendeleo na chama hakitamvumilia mvurugaji yoyote ndani ya chama

Chanzo: www.tanzaniaweb.live