Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chongolo: Chagueni wafia chama

C8aaa5e048570e599bc38de07a71829a Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo

Sun, 26 Jun 2022 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo amewataka wanachama wa CCM kuchagua viongozi wenye dhamira ya dhati ya kukipambania chama hicho ambao wapo tayari kukilinda chama na serikali yake kwa jasho na damu.

Chongolo alisema hayo mkoani Kigoma akiwa njiani kuelekea nchini Burundi ambapo atafanya ziara ya siku tatu nchini humo.

Pamoja na mambo mengine, anatazamiwa kufungua uwanja wa michezo na kituo cha kukuza vipaji unaojulikana kama Nkurunziza Peace Park Complex uliopo Mkoa wa Makamba nchini Burundi.

Alisema katika uchaguzi huu wa viongozi wa ndani ya CCM ni lazima wapiga kura wazingatie kuchagua viongozi wenye mapenzi ya kweli kwa chama ambao ndio msingi wa viongozi wa serikali kwa siku zijazo.

“Ni lazima kuzingatia uchaguzi wa viongozi ambao wanaonekana kuwa na dhamira za kuwatumikia wananchi. Mkikosea sasa mtakuwa mmekosea kwa miaka yote, hivyo umakini katika uchaguzi wa kiongozi anayefaa ufanyike sasa na kwa umakini mkubwa," alisema Chongolo.

Alisema wapo wagombea wenye hila ambao wanawania nafasi za uongozi ndani ya chama kwa dhamira zao binafsi na kwamba ni vizuri wapiga kura wakaliona jambo hilo na kuwaweka kando wagombea hao.

Chongolo anafanya ziara nchini Burundi kwa mwaliko wa Chama cha CNDD – FDD ambapo safari yake itamfikisha hadi Bujumbura, mji mkuu wa Burundi ambako atakutana na viongozi wa chama hicho na serikali ya Burundi.

Chanzo: www.habarileo.co.tz