Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chiza apitishwa kugombea ubunge Buyungu

11192 Chiza+pic TanzaniaWeb

Tue, 10 Jul 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam.Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimemteua Christopher Chiza kuwa mgombea wa ubunge jimbo la Buyungu mkoani Kigoma kwa tiketi ya chama hicho.

Taarifa iliyotolewa leo, Jumanne Julai 10, 2018 kwa vyombo vya habari na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole imesema Chiza ameteuliwa na Kamati Kuu ya CCM iliyokutana leo chini ya mwenyekiti wake Rais John Magufuli.

Chiza ambaye aliwahi kuwa mbunge wa jimbo hilo anagombea kwa mara nyingine baada ya kuangushwa katika uchaguzi mkuu wa 2015 na marehemu Kasuku Bilago wa Chadema.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya Polepole, pamoja na mambo mengine kwa kauli moja Kamati Kuu imempongeza Rais Magufuli  kwa utekelezaji mzuri wa Ilani ya uchaguzi ya CCM na kwa kasi kubwa ya upelekaji maendeleo na huduma za kijamii hasa katika maeneo ya pembezoni na mijini.

Pia wajumbe wa kamati hiyo kwa pamoja wameridhishwa na kuweka kauli kwamba jitihada hizo za kuongeza tija, ufanisi, faida, utumishi wa watu, uadilifu, vita dhidi ya rushwa na kupambana na ubadhirifu wa mali za chama na umma na uchapakazi kwenye chama na Serikali ziendelezwe maradufu.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz