Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chauma chajipanga uchaguzi Serikali za Mitaa, Rungwe ahimiza Watanzania

80986 Chauma++pic Chauma chajipanga uchaguzi Serikali za Mitaa, Rungwe ahimiza Watanzania

Mon, 21 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chama cha Ukombozi wa Umma (Chauma), Hashimu Rungwe amesema licha ya changamoto mbalimbali ikiwamo ya  kuzuiliwa mikutano ya hadhara, chama hicho hakitasusia uchaguzi ujao wa Serikali za mitaa.

Amesema uchaguzi huo ni muhimu hivyo kama wataususia, watawanyima haki wananchi ya kupata viongozi bora na wanaowahitaji.

Rungwe ameyasema hayo leo Jumapili Oktoba 20, 2019 katika mkutano wake na waandishi wa habari akilenga  kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura.

“Sisi hatutasusia na wala hatuna mpango huo kwa sababu huu ni uchaguzi muhimu sana kwa wananchi na si wa mtu binafsi wala chama binafsi, hivyo kila chama kina haki ya kushiriki kwa kuwa kinatambulika katika ofisi ya msajili wa vyama,” amesema Rungwe.

Amesema chama hicho kimejipanga kuweka mgombea kila mtaa katika mikoa yote nchini.

“Mapema Oktoba 29, wagombea wetu wataenda kuchukua fomu wajaze na kuzirejesha ili michakato mingine iendelee, kwa hiyo tunaomba wajitokeze kwa wingi kuwania nafasi hizo hasa wanawake,” amesema mwenyekiti huyo.

Pia Soma

Advertisement
 

Chanzo: mwananchi.co.tz