Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Changamoto zilizoyokea uchaguzi 2020 zilivunja rekodi - Warioba

Warioba (2) Changamoto zilizoyokea uchaguzi 2020 zilivunja rekodi - Warioba

Tue, 12 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyewahi kuwa Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais, Joseph Warioba, ameonyesha kukerwa na changamoto zilizojitokeza katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020, huku akisema mambo hayo yalikuwa mapya katika histori ya chaguzi nchini.

Jaji Warioba ameyasema hayo leo Jumanne Septemba 12, 2023, wakati akitoa mchango wake kwenye mkutano wa wadau wa demokrasia nchini, ulioitishwa na Baraza la Vyama Vya Siasa, na kufunguliwa jana na Rais Samia Suluhu Hassan.

Kutokana na changamoto zilizojitokeza katika chaguzi zilizopita, Jaji warioba amesema alitarajia kuona zikifanyiwa kazi na Serikali, na hasa kisheria kwa sababu mambo yaliyofanyika yalikuwa wazi na watu wote waliona.

“Mwaka 2020, pamoja na mafanikio, kulikuwa na changamoto nyingi sana na kwa vyovyote vile, hata kama isingekuwa sasa, mimi nilitegemea angalau ndani ya Serikali, changamoto zile zilionekana na hatua zingechukuliwa ama kisheria au kikanuni au utaratibu kuepusha zisije zikatokea mwaka 2024 na 2025," amesema na kuongeza;

“Wote tunajua kilichotokea mwaka 2019 na 2020, ilikuwa mara ya kwanza, Watanzania wamezoea kupiga kura, huwa zinatokea changamoto lakini siyo kama ilivyokuwa mwaka 2020, ilikuwa mara ya kwanza kwa wagombea wengi kuenguliwa kwenye uchaguzi, tuliona matumizi makubwa ya fedha katika kila hatua kuanzia kwenye uteuzi hadi kampeni.”

Jaji Warioba amesistiza: "Kama wanataka kuepusha hayo yaliyotekea huko nyuma, basi ni vema wakajiandaa kwa kuangalia sheria, kanuni na hasa taratibu za kusimamia uchaguzi ili wasipate matatizo kwenye uchaguzi ujao."

Jaji Warioba anaamini kuwa hayo yasipofanyika, yatasababisha watu wasiende kupiga kura kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live