Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chama cha CCM kiyafanyie kazi haya haraka kabla ya 2020

69799 Ccm+pic

Mon, 5 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Uhalali wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kuendelea kupata kibali kwa Watanzania kuendelea kuongoza serikali, unaweza kuwa katika vipimo tofauti vya mizani.

Kipimo ambacho CCM inakitazama kama mtaji imekuwa ni utekelezaji wa ahadi zake za mwaka 2015, kupitia Ilani ya 2015/2020.

Ahadi zilizopo katika Ilani hiyo zilimwezesha John Magufuli kuibuka mshindi wa urais katika uchaguzi huo kwa kupata kura 8,882,935 sawa na asilimia 58.46 huku Edward Lowassa wa Chadema kupitia Ukawa akipata kura 6,072,848 sawa na asilimia 39.97. Lowassa kwa sasa amrejea CCM.

Kwa mujibu wa CCM, Rais John Magufuli anayetekeleza ahadi hiyo amefanikiwa kwa kiwango kikubwa katika awamu yake ya kwanza ya miaka mitano inayomalizika mwakani huku akiwa tayari kuingia kwenye kinyang’anyiro cha kutetea kiti chake kwa awamu ya pili na ya mwisho kwa mujibu wa Katiba.

Baadhi ya mitaji ya chama hicho kuelekea uchaguzi ujao wa mwaka 2020 inatazamiwa kuwa ni pamoja na utekelezaji wa miradi mikubwa ya ujenzi wa madaraja, barabara za lami, Reli ya Kisasa (SGR), mradi wa umeme wa Mto Rufiji, Elimu bure na kukuza sekta ya usafiri wa anga.

Hata hivyo, yako mambo sita ambayo CCM inatakiwa kuyatafutia ufumbuzi haraka ili kujisafishia njia zaidi kabla ya kupulizwa kipenga cha kuelekea kampeni za Uchaguzi Mkuu ujao 2020.

Pia Soma

Maeneo hayo yanayogusa ndani na nje ya chama hicho ni pamoja na ahadi ya Sh50milioni kwa kila kijiji, migogoro wa ndani ya chama, nyongeza ya mishahara kwa wafanyakazi, matukio ya utekaji, malalamiko ya upinzani na hoja ya ugumu wa maisha.

Wachambuzi wa duru za kisiasa wanasema huenda maeneo hayo yakaonekana mwiba unaoweza kupunguza nguvu ya mtaji iliyowekeza kupitia utendaji wa kazi za Rais Magufuli.

 

Kwa habari zaidi soma gazeti la Mwananchi la leo Jumapili Agosti 4, 2019

Chanzo: mwananchi.co.tz