Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chama cha ADC chasimamisha mgombea uspika wa bunge

8da0f6569591e8da6735c3c41493cbaf Chama cha ADC chasimamisha mgombea uspika wa bunge

Sun, 16 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchakato wa uchukuaji fomu kugombea nafasi ya Spika wa Bunge unazidi kushika kasi, baada ya leo Januari 16, Chama Cha Alliance for Democratic Change (ADC) kumsimamisha mwanachama wao mmoja kugombea nafasi hiyo kwa kuchukua fomu.

Mwanachama huyo mwenye shahada ya kwanza ya sayansi ya siasa na utawala wa umma aliyejitambulisha kwa jina la Maimuna Kassim amekuwa wa kwanza kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa kukiwakilisha chama hicho katika nafasi hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya chama hicho yaliyopo Buguruni Dar es Salaam, Maimuna amesema ilikuwa ni ndoto yake kugombea nafasi hiyo na hakuona haja ya kusita baada ya kuwa na vigezo vyote.

Mwanachama huyo wa aliwahi kugombea ubunge katika jimbo la Kilindi mkoani Pwani katika uchaguzi wa mwaka 2020.

Maimuna amekabidhiwa fomu hiyo na Kaimu Naibu Katibu Mkuu Bara, Doni Mnyamani ambapo gharama za fomu hiyo ni Sh100, 000.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live