Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chalamila asema sijiuzulu uenyekiti wa CCM ng’oo

11075 Chalamila+pic TanzaniaWeb

Thu, 9 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mbeya. Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila ametoa msimamo wake akisema hawezi kujiuzulu uenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa kutokana na baadhi ya wanachama wa CCM kuanza kumshinikiza kuachia wadhifa huo.

Amesema alianza kupata shinikizo hilo kutokana na utaratibu mpya wa CCM, wa mtu mmoja kuwa na cheo kimoja.

Chalamila ametoa msimamo huo leo Agosti 9 wakati akizungumza na viongozi wa dini Ukumbi wa Mkapa jijini hapa alipokutana nao kwa lengo la kuwekana sawa katika shughuli za kuendesha mkoa huo.

 “Nilipoteuliwa ukuu wa Mkoa wa Mbeya, mtu mmoja akasema sasa natakiwa kujiuzulu uenyekiti. Nikasema sijiuzulu huu uenyekiti, kwa vile Rais ameniteua kuwa Mkuu wa Mkoa huku akijua mimi ni mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa. Ila nitajiuzulu kwa maelekezo ya Rais aliyenitua ukuu wa mkoa,” amesema Chalamila.

Mbali na hilo, Chalamila amesema kuna kipindi nchi ilianza kubaguana kwa misingi ya kisiasa jambo halikuwa na tija kwa afya ya mustakabali wa maendeleo ya nchi.

“Naombeni sana ushirikiano mkubwa na wa karibu muda wote na viongozi wa dini na taasisi zake. Tusibaguane kwa misingi ya kidini na badala yake tuungane kwa misingi ya dini zetu. Ilifika mahala nchi ilianza kubaguana kwa misingi ya kisasa,” amesema.

Soma Zaidi:

Mwenyekiti CCM Iringa aweka hadharani sababu za kufanya vibaya

 

Chanzo: mwananchi.co.tz