Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chadema yazindua sera mpya

19250 Chadema+pic TanzaniaWeb

Tue, 25 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es salaam. Chadema imezidua sera mpya ya mwaka 2018 iliyogawanyika kwenye maeneo matatu.

Akizungumza leo Septemba 25, 2018 wakati wa uzinduzi huo, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema sera hizo zitakuwa zinafanyiwa marekebisho kulingana na wakati.

Amesema eneo la kwanza lililoko kwenye sera hiyo ni ile inayolinda uhuru wa wananchi.

Mbowe amesema Mwalimu Julius Nyerere aliwahi kuzungumzia suala la maendeleo ya watu na uhuru, jambo ambalo wamelijadili kwa kina kwenye sera hiyo.

Amelitaja eneo lingine ni nafasi kuwa na sera zinazolenga misingi ya uchumi.

Amesema katika eneo hilo wameainisha ni kwa namna gani wananchi watapata huduma za kijamii.

Amefafanua eneo hilo limeainisha namna uchumi utakavyokuwa endelevu badala ya kuwa uliohodhiwa na Serikali.

Mbowe ameitaja sera nyingine ni zinazoilinda na kuihuisha jamii kupata huduma ya maji, barabara yasiwe mambo yanayofanywa na sekta binafsi bali yafanywe na Serikali.

"Sasa hivi kumejengeka dhana kuwa Serikali uliyojenga shule, zahanati inakuwa ni kama msaada, hii si sawa hayo ni majukumu ya Serikali," amesema Mbowe.

Mbowe amesema kabla ya kutayarisha sera hiyo wametumia mwaka mzima kufanya tafiti na kukusanya maoni kutoka kwa watu mbalimbali.

Chanzo: mwananchi.co.tz