Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chadema yatangaza wagombea majimbo 163

5b182909a3a5e7d30d88ba62fed35a79 Chadema yatangaza wagombea majimbo 163

Mon, 10 Aug 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetangaza awamu ya kwanza ya majina ya wagombea ubunge wa chama hicho kwa majimbo 163 kutoka kanda 8 za Tanzania bara.

Akitangaza matokeo hayo jijini Dar es Salaam jana, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema bara, Benson Kigaila alisema awamu hiyo ya kwanza imejumuisha kanda nane kati ya kumi zilizogawanywa kwa mfumo wa chama hicho zikiwa na jumla ya majimbo 163 kati ya majimbo 214 ya Tanzania bara.

“Tanzania ina jumla ya majimbo 264, Bara ina majimbo 214 na Zanzibar majimbo 50. Katika mfumo wetu wa kichama tumegawanya majimbo hayo katika kanda kumi, nane zikiwa ni za Tanzania bara na mbili ni za Zanzibar, leo tunaanza kutangaza majimbo 163 kwa kutaja kanda moja moja za Tanzania bara,” alisema Kagaila.

Alitaja kanda hizo zinazojumuisha majimbo 163 kuwa ni Pwani, Kaskazini, Kusini, Victoria, Serengeti, Magharibi, Nyasa na Kati.

Miongoni mwa waliopitishwa kugombea ni Asia Msangi (Ukonga), John Mrema (Segerea), Halima Mdee (Kawe), Boniface Jacob (Ubungo). Wengine ni Rebeka Mngodo (Arumeru Mashariki), Cesilia Pareso (Karatu), Godbless Lema (Arusha Mjini), Freeman Mbowe (Hai), Lucy Ndesamburo (Moshi Vijijini), Grace Kiwelu (Vunjo), Nagenjwa kaboyoka (Same Mashariki), Mathayo Gekuru (Babati Vijijini), Ali Gadaffi (Tanga Mjini) , Juma Bendera (Mkinga), na Zainab Ashraf (Pangani).

Wengine ni Abasi Mayala (Buchosa), Upendo Peneza (Geita Mjini), Masai Machae (Chato), Esther Bulaya (Bunda Mjini), Mwita Megabe (Bunda Vijijini) Esther Matiko (Tarime Mjini), John Heche (Tarime Vijijini), Catherine Ruge (Serengeti), Ezekia Wenje (Rorya), Julius Mwita (Musoma Mjini), na Florence Njugu (Musoma Vijijini).

Wagombea wengine ni Felix Mkosamali (Muhambwe), Ashura Mashaka (Buyungu), Loda Kunchela (Mpanda Mjini), Msuka Msuka (Katavi), Iddi Faraji (Msimbo), Stephan Hamisi (Kavuu), na Emannuel Mbuba (Ileje).

Wengine ni Frank Mwakwajoka (Tunduma), Paschal Haonga (Mbozi), Joseph Mbilinyi (Mbeya Mjini), Sophia Mwakagenda (Rungwe), Grace Tendega (Kalenga), Patrick Sosopi (Isimani), Peter Msigwa (Iringa Mjini), July Mpugula (Kilolo), Devotha Minja (Moro Mjini), Joseph Haule (Mikumi), Suzan Kiwanga (Mlimba), na Jesca Kishoa (Iramba Magharibi Akizungumzia mchakato huo Kagaila alisema chama hicho kinafanya uamuzi kwa mkakati wa ndani ni nani wamchague na kwa sababu gani ndiyo sababu baadhi ya wagombea ambao walipita wakati wa kura za maoni wameenguliwa katika uteuzi huo.

Chanzo: habarileo.co.tz