Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chadema yashinda Nkasi Kaskazini

C39771bbb7e146d085948a05949766b9 Chadema yashinda Nkasi Kaskazini

Fri, 30 Oct 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

Msimamizi wa Uchaguzi jimbo la Nkasi Kaskazini, amemtangaza Aida Khenani wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuwa ndiye mbunge wa jimbo hilo baada ya kupata kura 21,226, na kumshinda Ally Keissy wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) aliyepata kura 19,972 hivyo kuwa mgombea wa kwanza kukitetea chama chake katika nafasi hiyo.

Aida Khenani kabla ya Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuvunjwa, alikuwa ni Mbunge wa Viti Maalum kuanzia mwaka 2015 hadi 2020 kupitia chama chake cha CHADEMA.

Mbali na CHADEMA kupata mtetezi wake wa kwanza Bungeni, mpaka sasa Chama cha Wananchi (CUF) kina mwakilishi mmoja wa Jimbo la Mtwara Vijijini, ambaye ni Shamsia Mtamba, aliyepata kura 26,262 na kumshinda aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kupitia CCM Hawa Ghasia aliyepata kura 18,505.

Katika matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 28 mwaka huu, mpaka sasa vyama vya upinzani yaani CHADEMA na kile cha CUF kina wawakilishi wawili pekee wa ubunge ambao tayari wamekwishatangazwa, huku wabunge wengine wa vyama vya upinzani wakishindwa kutetea majimbo yao ambayo kwa asilimia kubwa yamechukuliwa na CCM.

Chanzo: habarileo.co.tz