Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chadema yamteua Munanka kuwania udiwani Turwa

Wed, 11 Jul 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Tarime. Chadema mkoani Mara, imemteua Charles Munanka kuwania udiwani Kata ya Turwa, katika uchaguzi mdogo utakaofanyika Agosti 12 mwaka huu.

Msimamizi wa mchakato huo, Amos Chilemba amesema Mnanka amepata nafasi hiyo baada ya kupata kura 40.

Wengine waliowania kupeperusha bendera ya Chadema ni Emmanuel Sasita , Debora Romeo na Nyankoba Kinyara .

Munanka anasubiri kuchuana na wagombea wa vyama vingine akiwamo  wa  CCM kujaza nafasi iliyobaki wazi baada ya aliyekuwa diwani wa kata hiyo, Zakayo Chacha kujivua uanachama wa Chadema na kujiunga CCM kwa kile alichosema ni kuridhishwa na kuunga mkono kazi zinazofanywa na Rais John Magufuli.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz