Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chadema yakamilisha uteuzi makatibu kanda nne

98680 Pic+makatibu Chadema yakamilisha uteuzi makatibu kanda nne

Wed, 11 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimekamilisha uteuzi wa makatibu wa kanda nne zilizokuwa zimebaki kukamilisha kanda kumi za chama hicho. Uteuzi huo umefanywa Jumatatu Machi 09, 2020 na kikao cha kamati kuu kilichofanyika jijini Dar es Salaam chini ya mwenyekiti wa chama hicho kikuu cha upinzani nchini humo, Freeman Mbowe. Taarifa iliyotolewa leo Jumatano Machi, 11, 2020 na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Chadema, Tumain Makene imewataja walioteuliwa na kanda zao kwenye mabano ni; Zacharia Obad (Viktoria,), Jackson Mnyawani (Serengeti), Ali Makame Zubeir (Unguja) na Habibu Ali Khamis (Pemba). Uteuzi wa makatibu hao unakamilisha nafasi kumi baada ya makatibu wa kanda sita kuteuliwa mwezi Februari. “Uteuzi wa makatibu wane ulianza Machi 10 pamoja na makatibu wa kanda zingine 6 walioteuliwa mwezi uliopita unakamilisha idadi ya makatibu 10 wa kanda zote za chama” imesema sehemu ya taarifa hiyo Awali chama hicho kilitangaza uteuzi wa makatibu katika kanda sita kikisema makatibu wa kanda nne watatangazwa badaye. Katika uteuzi huo wa mwezi Februari walioteuliwa pamoja na kanda zao kwenye mabano; Amani Golugwa (Kaskazini), General Kaduma (Kusini) na Ali Hemed (Pwani). Makatibu wengine walioteuliwa ni; Emmanuel Masonga (Nyasa), Gwamaka Mbughi (Kati) na Kangeta Kangeta (Magharibi).

Chanzo: mwananchi.co.tz