Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chadema yaeleza mkakati Uchaguzi Mkuu, kuunda baraza la Bavicha Queen

90895 Pic+chadema Chadema yaeleza mkakati Uchaguzi Mkuu, kuunda baraza la Bavicha Queen

Mon, 6 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanza. Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Taifa Chadema (Bavicha), nchini Tanzania, John Pambalu amesema baraza hilo linajipanga kufanya ziara nchi zima kuhamasisha vijana kwenye mapambano ya kuleta mapinduzi ya chama hicho kushika dola nchi inapoelekea kwenye Uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu.

Pambalu ametoa kauli hiyo leo Jumapili Januari 5, 2020, baada ya kupokewa katika ofisi za Kanda Victoria jijini Mwanza.

Amesema nchi yoyote duniani inayopambania mapinduzi lazima uwahusishe vijana.

“Ofisi ya Katibu Mkuu inaratibu ziara hiyo, na muziki tutakaouwasha Taifa zima litajua nini maana yetu na tutaanzia Dar es Salaam,” amesema.

 

Ili kufanikisha kazi hiyo, Pambalu amewaagiza viongozi wote kuanzia ngazi ya kata hadi wilaya kubainisha changamoto zote zilizopo kwenye maeneo yao ili kuziwasilisha kwenye chama.

Pia, amesema baraza hilo lina mkakati wa kuandaa baraza la vijana hususani wasichana wenye umri kati ya miaka 18 hadi  25 ili kujiunga na chama hicho kupigania mapinduzi.

Amerudia kauli yake kwamba Bavicha watahakikisha wanatumia kila njia bila woga wala hofu kudai Tume huru ya uchaguzi.

“Tunaomba katika hili kuungwa mkono hata kama ni mwanaCCM, mapinduzi ya kweli yanahitaji uungwaji mkono,” amesema Pambalu.

Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Pamela Maasai amewataka kuunganisha nguvu zao pamoja katika mapambano hayo badala ya kumuangalia mtu mmoja apiganie nguvu ya umma, huku akisema chama hicho kinaimani kubwa na vijana.

Chanzo: mwananchi.co.tz