Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chadema yaanza kusuka safu ya uongozi

33489 Pic+chadema Tanzania Web Photo

Wed, 26 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Vumbi la uchaguzi ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) limeanza kutimka katika maeneo mbalimbali ya nchi huku kikiwa kimepanga safu ya viongozi kwenye maeneo hayo kwaajili ya kusimamia chaguzi hizo.

Uchaguzi huo unahusisha viongozi wa matawi, Kata, majimbo, mikoa na ngazi ya Kitaifa ulianza mapema mwezi huu ambapo wabunge wa Chadema wamegawana maeneo mbalimbali ya kusimamia.

Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano, Uenezi na Mambo ya Nje wa Chadema John Mrema alipozungumza na Mwananchi alisema uchaguzi huo unaenda sambamba na vikao vya ndani kwaajili ya wagombea kupata nafasi ya kujinadi.

Anasema kutokana na kuzuiwa kwa mikutano ya hadhara nchini uchaguzi huo unatumia vikao vya ndani ambavyo hatahivyo katika baadhi ya maeneoe vimekuwa kaa la moto.

Chadema kimewatumia viongozi wenye ushawishi mkubwa wakiwamo wabunge kuongoza zoezi hilo.

Desemba 16, 2018 Naibu Katibu Mkuu wa Chadema-Zanzibar, Salum Mwalimu alikamatwa na Jeshi la Poilisi akiwa mjini Mafinga mkoani Iringa alikokwenda kushiriki moja ya kikao cha ndani akitokea Kanda ya Nyasa.

Mrema alisema Kiongozi huyo ni moja ya safu iliyopangwa kusimamia chaguzi hizo katika majimbo ya Makambako, Makete, Ismani na Iringa Mjini.

Huu ni mwaka wa uchaguzi ndani ya Chama na ndio maana tuko nchi nzima, tumesambaa kwa ajili ya kusimamia ili tuweze kuapata vipongozi wazuri kuanzia ngazi ya msingi,” alisema Mrema.

Wakati Mbunge wa Kibamba, John Mnyika akishika majimbo ya Momba, Tunduma, Vwawa, Mbeya Mjini na Vijijini, Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa anasimamia majimbo yote ya mkoa wa Rukwa.

Mbunge wa Mbeya mjini, Jospeh Mbilinyi maarufu kama ‘Sugu’ anasimamia jimbo la Njombe Mjini.

Mrema alisema uchaguzi huo umefikia ngazi tofauti ambapo Kanda ya Kaskazini katika jimbo la Serengeti na Victoria wamemaliza kuchagua viongozi wa ngazi ya majimbo.

“Uchaguzi wa ndani ya chama wagombea wanapewa fursa ya kujitangaza na kwa sababu wanagombea kuanzia ngazi ya Kitongoji, kiongozi anaenda kujinadi kwenye kikao cha uchaguzi,” alisema.

Anasema kwa mkoa wa Dar es Salaam uchaguzi huo umefikia ngazi ya viongozi wa Majimbo huku Kanda ya Nyasa ikiwa katika ngazi ya Kitongoji.

Hata hivyo, anaeleza kuwa chaguzi hizo zinakumbana na kashikashi mbalimbali ikiwamo baadhi ya viongozi kukamatwa na Jeshi la Polisi wakati wakiendesha vikao vya ndani.

Mbali na Naibu Katibu Mkuu-Zanzibar Salum Mwalimu ambaye aliyekamatwa Desemba 16 akiwa Mjini Mafinga wapo viongozi wengine ambao walikamatwa wakiwamo wasimamizi wa uchaguzi katika Jimbo la Bunda.



Chanzo: mwananchi.co.tz