Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chadema watangaza awamu ya pili ya maandamano

Chadema Watangaza Awamu Ya Pili Ya Maandamano Chadema watangaza awamu ya pili ya maandamano

Thu, 1 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetangaza ratiba ya awamu ya pili ya maandamano yatakayoanzia mkoani Mwanza Februari 13, 2024 kisha kuelekea katika majiji ya Arusha na Mbeya.

Tayari Chadema wameshafanya awamu ya kwanza ya maandamano yaliyofanyika Januari 24, 2024 jijini Dar es Salaam yakilenga kushinikiza Serikali kuondoa bungeni miswada mitatu ya sheria za uchaguzi inayotarajiwa kupitishwa kesho. Miswada hiyo inaendelea kujadiliwa na wabunge.

Pia wanaitaka Serikali kupeleka mpango wa dharura wa kukwamua hali ya ugumu wa maisha wanaopitia Tanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Februari mosi, 2024 jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika ametaja tarehe za maandamano hayo kwa jiji la Mbeya kuwa Februari 20, 2024 na Jiji la Arusha Februari 27, 2024 akisema maandalizi ya maandamamano hayo yanaendelea.

Amesema msukumo wa maandamano hayo nchi nzima unaendelea kwa kuwa baada ya kufanya Dar es Salaam, hakuna kiongozi wa Serikali aliyetoka kutoa kauli yeyote.

"Kutokutoka kwa umma kwa kiongozi yeyote mwandamizi serikalini kuzungumza chochote tunachukulia ni muendelezo wa kupuuza maoni ya wananchi, ndiyo maana tumekuja kutangaza tena na safari hii tunakwenda kwenye majiji matatu hadi Serikali itakaposikiliza," amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live