Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chadema washauri kuanzishwa taasisi huru kukabili maafa

Chademapic Kutoshiriki Chadema washauri kuanzishwa taasisi huru kukabili maafa

Tue, 8 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Siku mbili baada ya ajali ya ndege ya Precision Air iliyoanguka Mkoa wa Kagera na kusababisha vifo vya watu 19, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimependekeza kitengo cha maafa kilichopo chini ya ofisi ya Waziri Mkuu kuvunjwa.

Ajali hiyo ilitokea asubuhi ya juzi Jumapili, Novemba 6, 2022 baada ya ndege hiyo iliyokuwa ikitoka jijini Dar es Salaam, kuanguka Ziwa Victoria ikiwa na watu 43 kati yao 39 abiria, wawili marubani na wawili wahudumu wa ndege.

Mapendekezo hayo yametolewa leo Jumanne Novemba 8, 2022 na mkurugenzi wa mawasiliano, itifaki na mambo ya nje, John Mrema wakati akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam.

Mrema amesema ni wakati wa Serikali kuunda taasi itakayokuwa chini ya Wizara ya Ulinzi itakayoitwa Tanzania Emergency Management Agency (TEMA) ambapo itakayokuwa na mamlaka kamili.

"Taasisi hii iongozwe na Jeshi la Wananchi (JWTZ) na iwe na jukumu la kuandaa jamii namna ya kujikinga na majanga, kuwa na wajibu wa kuitika haraka panapotokea janga lolote na kuorodhesha watu wenye taaluma mbalimbali katika maeneo tofauti,"amesema Mrema.

Pia chama hicho kimependekeza kutengwe bajeti kwaajili ya kununua boti za uokoaji, helkopta za doria kwaajili ya uokoaji paamoja na kuwepo wazamiaji kwenye viwanja vilivyopakana na bahari au maziwa.

"Tunapendekeza pia kuwepo kwa taa kwenye barabara za kurukia ndege, mitambo mikubwa kwa ajili ya kunyanyua vitu vizito pamoja kutoa mafunzo yya uokoaji kwa jamii inayozunguka viwanja vya ndege," amesema.

Aidha, Mrema amesema chama hicho hakiridhishwi na jitihada zilizochukuliwa baada ya ajali kutokea na kushauri wahusika wote kuwajibika au wawajibishwe.

"Yapo maswali ya kujiuliza, kama rubani mara ya kwanza alitoa taarifa, kwa nini hakuna tahadhari yoyote iliyotolewa ikiwemo maandalizi ya vifaa vya uokoazi.

"Kama alitoa taarifa na mwongoza ndege alikuwa kazini baada ya rubani kumpa taarifa na yeye kwenda kuzunguka alichukua hatua gani?" amehoji.

Ameongeza kuwa hata wakati wa ukoaji vifaa mbalimbali ambavyo vingewezesha kutoa msaada kwa haraka ikiwemo mitambo ya kunyanyua vitu vizito na maboya

Chanzo: www.tanzaniaweb.live