Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chadema wamlilia Mtanzania aliyefia vitani Russia

Chadema Wamlilia Mtanzania Aliyefia Vitani Russia Chadema wamlilia Mtanzania aliyefia vitani Russia

Fri, 27 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema kada wake, Nemes Tarimo aliyefia vitani nchini Ukraine akitetea masilahi ya Russia, atakumbukwa kwa harakati za kutafuta uhuru, haki na Demokrasia ya Maendeleo ya watu.

Kada huyo alifariki dunia Oktoba mwaka jana, alikuwa mwanachama na kada wa Chadema na mwaka 2020 aliomba nafasi ya kuwania ubunge wa Jimbo la Kibamba na kushika nafasi ya tatu kwenye mchakato wa kura za maoni ndani ya Chadema.

Akizungumza Dar es Salaam kwenye msiba huo, Mwenyekiti wa Jimbo la Kibamba Ernest Mgaya, amesema ndiyo utaratibu wao siku zote mwanachama anapopata matatizo chama kushiriki.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live